Saturday, 10 June 2017

TAMISEMI YATANGAZA WATAKAO JIUNGA KIDATO CHA TANO 2017/2018


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi) George Simbachawene ametoa idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano na vyuo vya ufundi kwa mwaka 2017 huku jumla ya wanafunzi 2,999 wakiachwa.

Simbachawene ametoa kauli hiyo leo mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi ws habari na kusema kuwa ufaulu kwa mwaka huu umeongezeka kwa asilimia 3.75 ukilinganisha na matokeo ya mwaka 2015.

Waziri amedai kati ya wanafunzi 96,018 waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu ni wanafunzi 93,019 tu ndiyo waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi.

Waziri Simbachawene amesema kuwa jumla ya watahiniwa wote waliofanya mtihani wa kidato cha nne kwa shule kwa mwaka 2016 ni 349,524 huku waliofanya mtihani wa kujitegemea ni 47,751 ambapo watahiniwa waliofanya mtihani wa shule waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60 ya watahiniwa waliofanya mtihani Tanzania Bara.

Simbachawene alisema kutokana na mwongozo wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wa Mei 15, 2017 jumla ya wanafunzi 93,019 ndiyo wenye Sifa za kuchaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi kwa kuwa wamefaulu vigezo vyote vya msingi kama vilivyoaibishwa na Wizara ya elimu sayansi na teknolojia ambapo kati ya hao 92,998 ni wa shule na wanafunzi 21 ni wale waliosoma taasisi ya elimu ya watu wazima.

Aidha amewataka wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano kuwasili kwa wakati katika shule walizopangiwa July 17 mwaka huu na kwamba hakutakuwa na mabadiliko ya shule walizopangiwa.

"Na kama kuna mwanafunzi ambaye hataripoti kwenye shule aliyopangiwa kwa muda wa siku 14 nafasi yake itachukuliwa na mtu mwingine," alisema Simbachawene.

Kuangalia majina ya wanafunzi na shule walizochaguliwa 

Thursday, 13 April 2017

MAJINA YA WALIMU WA SAYANSI WALIOPATA AJIRA



SeeBait
Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI imetangaza ajira mpya kwa Walimu wa masomo ya Hisabati na Sayansi leo tarehe 12 Aprili, 2017.

Majina ya Walimu yaliyotangazwa yanatokana na tangazo la nafasi ya kazi ya Ualimu lililotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia mnamo tarehe 01 Desemba, 2016.
 
Jumla ya Walimu wapya wapatao 3,081 wakiwemo 1,544 ni wa ngazi ya Shahada na Walimu 1,537 ni wa Stashahada.
 
Walimu hao watatakiwa kuripoti kwenye Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri na baadaye kwenye Shule walizopangiwa kuanzia tarehe 18 Aprili, 2017 hadi tarehe 25 Aprili, 2017. Walimu wote waripoti wakiwa na vyeti halisi vya taaluma vya kidato cha nne (IV) na kidato cha sita (VI), vyeti halisi vya kitaalaam vya kuhitimu mafunzo ya Ualimu ngazi ya Stashahada na Shahada na Cheti cha kuzaliwa.
 
Angalizo :
i. Walimu waliopangiwa vituo ni wa masomo ya Hisabati na Sayansi waliohitimu hadi mwaka 2014/2015.

ii. Kituo cha kazi cha mwalimu ni shule aliyopangiwa na sio makao makuu ya Halmashauri.
 
iii. Mwalimu atakayeripoti na kuchukua posho ya kujikimu na baadae kuondoka atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
 
iv. Walimu wote watakiwa kuripoti katika vituo vyao kuanzia tarehe 18 Aprili, 2017 hadi 25 Aprili, 2017, watakaochelewa nafasi zao zitajazwa na mwalimu mwingine.
 
v. Hakutakuwa na uhamisho ndani ya Mkoa au Halmashauri.
Majina ya Walimu hao yanapatikana katika tovuti ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz
 
Imetolewa na:
Katibu Mkuu
Ofisi ya Rais TAMISEMI

==>Orodha ya Walimu wa Shahada wa Ajira Mpya kwa Masomo ya Sayansi na Hisabati.



==>Orodha ya Walimu wa Ajira Mpya kwa Masomo ya Sayansi na Hisabati.

Wednesday, 5 April 2017

MBIO ZA UBINGWA ZA ZIDI KUNOGA ENGLAND


Bildergebnis für hazard

Magoli ya Eden Hazard ya dakika ya 10 na 35 yazidi kuiweka chelsea kileleni ikishinda nyumbani zidi ya mancherster city 2-1, huku Aguero akifunga bao pekee la mancherster city dakika ya 26. ushindi huu unaiweka chelsea kileleni point 7 juu ya tottenham walioko nafasi ya pili kwenye ligi hiyo.mechi nyingine,HULL CITY 4 - 2 MIDDLESBROUGH,SWANSEA CITY 1 - 3 TOTTENHAM
HOTSPUR,SOUTHAMPTON 3 - 1 CRYSTAL PALACE,LIVERPOOL 2 - 2 AFC BOURNEMOUTH.ARSENAL 3 - 0 WEST HAM UNITED.ligi itaendelea wikendi hii.

MATOKEO YA UCHAGUZI WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI(EALA)

Jana Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipiga kura kuchagua wabunge watakaoiwakilisha nchi katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) kwa kipindi cha miaka mitano.

Baada ya mvutano wa muda mrefu kuhusu uchaguzi huo, ulifanyika na Spika wa Bunge, Job Ndugai kutangaza orodha ya washindi waliochaguliwa kuiwakilisha nchi.

Tanzania inatakiwa kutoa wabunge 9 kwenda EALA, lakini matokeo ya jana yalitangaza washindi saba tu baada ya wagombea wawili kupigiwa kura nyingi za hapana, na hivyo kuonekana kuwa wabunge hawakuwataka.

Kati ya wabunge 7 waliotangazwa, 6 ni wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na mmoja na wa Chama cha Wananchi (CUF).

Wagombea wa CHADEMA, Lawrence Masha na Ezekiah Wenje walipingwa kwa kupigiwa kura nyingi za hapana.
  1.      Fancy Nkuhi (CCM)
  2.     Happiness Legiko (CCM)
  3.     Maryam Ussi Yahya (CCM)
  4.     Dkt Abdullah Makame (CCM)
  5.     Dkt Ngwaru Maghembe (CCM)
  6.     Alhaj Adam Kimbisa (CCM)
  7.     Habib Mnyaa (CUF)
Baada ya matokeo hayo kutangazwa, Mwenyekiti wa CHADEMA na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Bunge alisema kuwa, hawayakubali matokeo hayo na kuwa watakwenda mahakamani.

Mbowe pia amemtuhumu Rais Dkt Magufuli na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuhusika katika mchakato wa kuwakataa wagombea wa CHADEMA na kusema kuwa, wao hawatakubaliana na hilo kwa sababu Spika wa Bunge amekiuka kanuni za bunge, na uchaguzi wote ulikuwa na kasoro

Thursday, 30 March 2017

MWAKYEMBE SAKATA LA MAKONDA NA CLOUDS MEDIA

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe leo amezungumza na waandishi wa habari Mjini Dodoma mara baada ya kukaribishwa rasmi Wizarani hapo..

Baada ya maongezi aliruhusu mwaswali ambapo moja ya swali aliloulizwa na wanahabari ni kuhusu ripoti iliyoachwa na Waziri wa zamani Nape Nnauye kuhusu uchunguzi wa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kudaiwa kuvamia ofisi za Clouds Media huku akiwa na Askari wenye silaha.

Haya ni majibu aliyoyatoa>>>>>>>
"Wengi mnauliza nimeifanyia kazi gani ripoti ya Nape, mimi hiyo ripoti sijaiona na kama mwanasheria kwangu ni mwiko na sitapeleka taarifa ambayo haijakamilika.

"Kupitia vyombo vya habari taarifa imeeleza kuwa ushahidi ulitolewa na upande wa Clouds Media na mkakiri kuwa upande wa pili haukupatikana.
 
"Huwezi kuwa Hakimu kwenye suala lako wewe mwenyewe, kufanya hivyo ni ubatili kwahiyo hata mimi ningekuwa ni mwandishi wa habari ningesema hili jambo siliwezi kwakuwa linanihusu na mimi.

"Kanuni zinataka kusikiliza upande wa pili, sasa mmeshasema kitu kina upande mmoja alafu nimpelekee kiongozi wangu..NO, mimi kazi yangu ni kupata maelezo ya upande wa pili na nitapata.

"Hili jambo ni lakufa na kupona, yani niache kukutana na wakuu wa idara mbalimbali hapa kuhakikisha nakuza suala la sanaa na kuhakikisha vijana wetu hawaendelei kuibiwa nibaki kuhangaikia suala la ripoti.

"Mimi sikuapa kwa jambo hilo moja pekee lakini mimi ni mwanasheria mkongwe na nitahakikisha nalifuatilia lakini mimi sitaunda kamati katika jambo hilo.

"Lengo letu ni kuhakikisha hatutakuwa na matukio ya namna hiyo katika safari lakini tukitoka na kauli za papara tutakuwa tunajitafutia matatizo hapo mbeleni "

MAKONDA AHOJIWA NA KAMATI YA BUNGE


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda leo amefika mbele ya kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kufuatia wito wa Kamati hiyo kumtaka afike mbele ya kamati kujibu tuhuma zinazomkabili za kuingilia Haki, Uhuru na Madaraka ya Bunge kutokana na matashi aliyoyatoa mapema mwezi februari 2017 jijini Dar es Salaam yaliyokuwa na madai ya kudharau Bunge.

Wito wa kufika mbele ya Kamati hiyo unafuatia Azimio la Bunge lilitolewa tarehe 8 Februari 2017 ambapo Bunge liliazimia Mhe. Spika aweze kukubali Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Alexandra Mnyeti na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Mhe Paul Makonda wahojiwe kutokana na Matamshi yao ya Kudharau Bunge.

Friday, 24 March 2017

Bofya hapa kudownload UHURU BLOG<<<<Download>>>>>